Full-Width Version (true/false)


Dkt. Magufuli ampa 'rungu' Katibu Mkuu mpya wa CCMMwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa Dkt. Bashiru Ali Kakurwa kuitendea haki nafasi aliyoteuliwa CCM na jumuia zake zote bila ya kubagua. 

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo mbele ya wajumbe wa waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo leo ni siku ya pili tokea kilipoanza jana Mei 28, 2018 kilichofanyikia katika kumbi za Ikulu Jijini Dar es Salaam.

"Tumekupa dhamana hii katika kipindi kigumu na tumenong’ona na Makamu wa Mwenyekiti na Rais wa Zanzibar kwamba kazi hii nzuri uliyoifanya Tanzania Bara ikafanyike na Tanzania Zanzibar. Tumekupa jukumu hili tukiwa na matumaini makubwa kwamba yote uliyoyaona kwa miezi mitano sasa ukayafanyie kazi katika Chama chote na jumuia zake kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM", amesema Dkt. Magufuli.

Mbali na hilo, Mwenyekiti wa CCM ameipongeza Tume iliyoongozwa na Dkt. Bashiru Ali Kakurwa kwa kazi nzuri ya kizalendo yenye mapenzi mema kwa Chama Cha Mapinduzi na iliyofanyika kwa uadilifu mkubwa.

No comments

Powered by Blogger.