Full-Width Version (true/false)


DODOMA: TAKUKURU wadaka Polisi wanne kwa kupokea rushwa ya TZS milioni 5Askari wanne wa pori la akiba la Mkungunero Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh milioni 5 za wafugaji wa Kijiji cha Irkiushiboir Kata ya Makame Wilaya ya Kiteto mkoani Mnyara.

Akizungumza leo Jumanne Mei 22, 2018 Kamanda wa TAKUKURU wilayani Kiteto, Julius Chacha amesema askari hao wamekamatwa Mei 20, 2018 wakiwa na bunduki nne aina ya SMG huku wakiwa na mifugo 200.


Amewataja askari hao kuwa ni Godfrey Matheas, Martenus Mahoka, Augustino Sadiki na Aphrahimu Polepole.


Amebainisha kuwa baada ya mmoja wa wafugaji kuombwa rushwa na watu hao, uliwekwa mtego na kukamatwa askari hao wakiwa wamepokea kiasi hicho cha fedha na kwamba walikuwa na mifugo zaidi ya 200 mali ya familia saba za wilayani Kiteto.


“Mtego huo uliwekwa kabla ya askari hao kuikabidhi mifugo kwa wenyewe. Tuliwakamata wahusika wakiwa wameshikilia mifugo hiyo katika kitongoji cha Ilchura kijiji cha Irkiushiboir wilayani Kiteto,"amesema Chacha. 

 NB:Kwa sasa unaweza kupata habari zetu zote sehemu moja kwa kupitia App yetu.pakua sasa kupitia play store kwa kubonyeza >>>HAPA

No comments

Powered by Blogger.