Full-Width Version (true/false)


Dr. Bashiru hakuwahi kuvaa shati la CCM miaka 15Wasomi kutoka chuo kikuu Cha Dar es Salaam wamepongeza hatua ya chama hicho kumteua Dkt. Bashiru Ally kuwa Katibu Mkuu wa Chama Tawala CCM huku wakishangazwa na usiri aliokuwa nao Katibu huyo kwakudai kuwa miaka 15 tangu wamfahamu hawakuwahi kumuona akijihusisha na masuala yoyote ya chama 

Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast kinachorushwa na East Africa Radio, Mtaalamu wa Sayansi ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Benson Bana, amesema hakuwahi kumuona Dkt. Bashiru amevaa sare za chama wala kutembea na Ilani, lakini anaamini mitazamo yake inarandana na misimamo ya chama hicho kikongwe nchini Tanzania.

“Nimejuana naye kwa miaka 15 lakini sikuwahi kumuona akiwa amevaa sare za chama wala kutembea na ilani ya chama lakini ni ukweli kwamba Dkt. Bashiru ni Mwepesi kujifunza mambo mapya, misimamo yake na mitazamo yake inaendana na falsafa za chama cha mapinduzi tangu waasisi wake, Yeye ni mtu anayeamini katika ujamaa na ni muumini mzuri wa sera za mwalimu nyerere, naamini atafanya vizuri zaidi katika nafasi yake hii mpya, muda mwingi ametumia kufundisha masuala ya uongozi lakini sasa ni nafasi nzuri yakwenda kufanya kwa vitendo. ” amesema Dkt. Bana

Mwengine aliyesifia uteuzi huo ni Dkt. George Kahangwa ambaye amestaajabu kwa kuwa hakuwahi kumuona Dkt. Bashiru na harakati za CCM lakini ameweka wazi kuwa ni mtu makini ambaye ana uzoefu na masuala ya uongozi tangu akiwa mwanafunzi wa chuo.

Dkt. Bashiru Ally hapo Jana Mei 29, 2018 ametangazwa rasmi kurithi mikoba ya Katibu Mkuu Mstaafu Abdulrhaman Kinana, akitazamiwa kukumbana na mitihani kadhaa ikiwemo chaguzi ndogo za serikali za mtaa mwakani kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

No comments

Powered by Blogger.