Full-Width Version (true/false)


Ebola yasababisha vifo vya watu 17 Congo

Watu 17 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC.

Wizara ya afya imesema kuwa kesi 21 za Ebola ziliripotiwa ndani ya wiki tano na kusababisha vifo vya watu 17 katika eneo la Bikoro nchini DRC.

Kwa mujibu wa habari hatua za kuudhibiti ugonjwa huo zinaendelea kwani umekuwa ni hatari kwa jamii nzima wakiwemo wafanyakazi.

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa la WHO limetuma madaktari kusaidia kupambana na ugonjwa huo.

No comments

Powered by Blogger.