Full-Width Version (true/false)


Edinson Cavani athibitisha kuwa na bifu na Neymar


Mshambuliaji wa klabu ya PSG ya Ufaransa Edinson Cavani amethibitisha kuwa, waliwahi kuwa na tatizo na nyota mwenzake wa timu hiyo Neymar Jr, mwanzoni mwa msimu huu.

Wawili hao walionekana kutokuelewana haswa ndani ya uwanja kwenye matukio muhimu kama upigaji wa penalti ambapo kila mmoja alikuwa anataka kuwa mpigaji. Hata hivyo waliweka mambo sawa na kuisadia timu kushinda ubingwa wa Ligue 1.

"Ni kweli kwamba tulikuwa na tatizo wakati huo na Neymar lakini tulizungumza tukamaliza na sasa tuko sawa kwaajili ya klabu na sio kiu ya kushinda vitu binafsi'', alisema Cavani.

Neymar na Cavani waligombania kupiga penalti kwenye mchezo wa ligi kuu ya Ufaransa dhidi ya Dijon, ambapo PSG ilikuwa inaongoza kwa mabao 7-0 na tayari Cavani alikuwa ameshafunga mabao 2 hivyo angepiga angefunga 'Hat-trick.

Nyota huyo wa Brazil msimu huu hajaumaliza vizuri baada ya kuumia mguu wa kulia mapema mwezi Februari ambapo amekaa nje hadi mwisho wa msimu. Neymar huenda akarejea kucheza fainali za Kombe la Dunia na timu yake ya taifa Brazil.

No comments

Powered by Blogger.