Full-Width Version (true/false)


EFM Radio yatua rasmi Jijini Dodoma

 

KITUO cha Utangazaji cha Efm redio katika kuhakikisha kinaenda sanjari na maendeleo pamoja na mpango wa serikali wa kuhamia Jijini Dodoma, imewasha rasmi masafa yake leo Jijini humo ambapo inasikika kupitia masafa ya 92.5 fm. 

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Efm Radio na TV E, Bwana Dennis Busulwa, wameelekeza matangazo ya kituo hicho Jiji la Dodoma kwa kuangalia uhitaji wa jamii pamoja na maendeleo ya jiji katika kuhabarisha, kuburudisha pamoja na kuelimisha.

Bwana Busulwa amesema Vilevile Efm redio inatarajia kuwasha masafa yake katika mkoa wa Morogoro, Tabora, na Kigoma pamoja na mikoa mingine ili kuhakikisha watanzania wote wanapata matangazo yake.

Aidha, Efm redio inazidi kuishukuru serikali na wadau wake wote hususani wasikilizaji wake kwa kuendelea kuwaunga mkono pamoja na kuwaahidi wasikilizaji wake kutimiza wajibu wake uliojiwekea kama chombo cha habari pamoja na kufikisha matamasha yake hususani ya uwezeshaji katika kuendeleza uchumi pamoja na elimu katika jamii.

No comments

Powered by Blogger.