Full-Width Version (true/false)


“Eti Nini Wamekula Tena Rambirambi?..... Wakina nani Walikua Wanachangisha Zile Hela Kwani”- Nay wa Mitego

Tetesi ambazo zimekuwa zikiendelea kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusiana na rambirambi zilizotolewa kwenye msiba wa Marehemu Agnes Gerald Waya “Masogange” kusemekana kuwa rambirambi hizo zilizotolewa hazijawafikia wanafamilia wa Marehemu Agnes Masogange.

Inasemekana kuwa waigizaji wa Bongo Movie wamekula hela hizo za rambirambi zilizotakiwa kuwafikia familia wa Marehemu.

Nay wa Mitego kupitia account yake ya instagram ameandika caption ambayo inasemekana imewalenga waliochukua rambirambi hizo “Eti Niniiii.?! Wamekula tena RambiRambiiiii😳😳😭😭…?! Nooo Hapana una uhakika? Wakina nani walikua wanachangisha zile hela kwani? naomba majina yao”

No comments

Powered by Blogger.