Full-Width Version (true/false)


FAHAMU Baba wa Tupac alivyokuja kuishi TanzaniaAnaitwa Geronimo Pratt ambaye ni baba wa kiroho wa msanii nguli wa hip hop duniani, 2Pac Shakur, na pia ni member wa juu wa Black Panther nchini Marekani. 
 
Pratt alizaliwa tarehe 13 Septemba, 1947, tarehe ambayo mtoto wake Tupac Shakur alifariki katika hospitali ya Las Vegas baada ya kupigwa risasi.

Brad alikuwa mtu wa karibu sana wa mama yake 2Pac Shakur, Afeni Shakur na aliyekuwa mume wake, Mutulu Shakur. (Mutulu Shakur ni baba wa kambo wa 2Pac ambaye ndiye alimlea)
Prat aliingia jeshini na alikuwa miongoni mwa askari waliopigana vita ya Maekani na Vietnam, mara baada ya kutoka jeshini alichukua masomo ya Sayansi ya siasa, na hatimaye kujiunga na Black pather, kundi ambalo liliundwa na Wamarekani Weusi kwa ajili ya kujitetea haki zao, na kufanikiwa kupewa uongozi wa juu kwenye kundi hilo ambalo lilitikisa Marekani.

Mwaka 1968 Geronimo alienda jela kwa tuhuma za kumuua mwanamke mmoja ambaye alikuwa mwalimu wa shule akiwa supermarket na mume wake, ambaye alijeruhiwa, na kumtaja Geronimo ndiye aliyefanya mauaji hayo.

Wakili wa Geronimo alijaribu kumtetea mteja wake kwa kusema kuwa siku ya tukio mteja wake hakuwa eneo la tukio, na alikuwa umbali wa mile 350, hivyo hakuhusika na mauaji hayo, lakini mahakama ilimkuta na hatia na kumuhukumu kwenda jela.

Akiwa jela aliweza kusoma masomo ya sheria na kuhitimu ili kumpa nguvu ya kujitetea kwenye kesi yake.

Geronimo aliachiwa huru na kufutiwa kesi yake baada ya miaka 27 kukaa jela, mnamo mwaka 1997. Kesi yake ilifutwa baada ya kugundua kuwa shahidi alikuwa ni 'informat' wa FBI, hivyo ikaonekana ni kesi ya kutengenezwa.

Baada ya kuachiwa huru walifungua kesi dhidi ya FBI kwa kumfunga kimakosa, kesi ambayo pia alijaribu kumtetea rafiki yake mkubwa kwenye kundi la Black Panther, Mumia Abu-Jamal. Kina Geronimo walishinda kesi hiyo na kulipwa dola million 2.75 .

Baada ya hapo Geronimo alikuja kuishi Tanzania bila watu kujua historia yake na kwa siri kubwa juu ya utambulisho wake, kwani nchini Marekani aliaminika kuwa miongoni mwa watu hatari. Aliishi Tanzania mkoani Arusha mpaka alipofariki June 2, 2011 , na kuacha familia yake wakiwemo mke na watoto.Source:  2PacLegacy.net
Geronimo akiwa na 2Pac awakati yuko mdogo
Geronimo akiwa Arusha Tanzania

No comments

Powered by Blogger.