Full-Width Version (true/false)


Fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kuonyeshwa bure

FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Liverpool na Real Madrid itaonyeshwa bure kwenye YouTube Mei 26, mwaka huu kutoka Uwanja wa NSK Olimpijs mjini Kyiv, Ukraine.
BT Sport imekubali kuonyesha bure mechi za mwisho za michuano ya klabu Ulaya kwa wote, kikosi cha Jurgen Klopp kikimenyana na wakali wa Zinedine Zidane Mei 26.

Fainali ya Europa League pia baina ya Atletico Madrid na Marseille Mei 16 pia itaonyeshwa bure.

BT Sport ilivutia watazamaji Milioni 6.5 kwenye fainali ya mwaka jana kati ya Real Madrid na Juventus, lakini inatarajia idadi hiyo itaongezeka mwezi huu kutokana na kuhusisha timu ya England.

No comments

Powered by Blogger.