Full-Width Version (true/false)


Familia ya John Heche Yakataa Fidia ya Serikali

Chacha Suguta (27), ndugu wa Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche aliyefariki dunia akidaiwa kuchomwa kisu akiwa mikononi mwa polisi, alizikwa jana nyumbani kwao katika Kijiji cha Nyabitocho wilayani humo.

Ingawa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima aliyefika nyumbani kwa marehemu kuhani msiba aliahidi kuwa Serikali itashirikiana na familia katika msiba huo, hakuna kiongozi yeyote wa Serikali wala Jeshi la Polisi ngazi ya mkoa na wilaya aliyehudhuria mazishi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye ndiye pekee aliyekuwa kiongozi wa chama tawala wa ngazi ya juu aliyehudhuria mazishi hayo.

No comments

Powered by Blogger.