Full-Width Version (true/false)


Frank Lampard apata dili la ukochaMchezaji wa zamani wa timu a taifa ya Uingereza, Frank Lampard, amefanikiwa kupiga hatua ya kuingia kwenye kazi ya ukocha rasmi.

Lampard amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuifundisha klabu ya Derby County inayoshiriki ligi daraja la kwanza Uingereza.

“Ninafurahi kuthibitisha hatua yangu ya kwanza katika usimamizi na @dcfcofficial, klabu yenye utamaduni mkubwa na historia,” ameandika Lampard kwenye mtandao wake wa Instagram.


Lampard alistaafu kucheza soka mwaka 2016 huku akiwa tayari amewahi kucheza timu kama West Ham United, Swansea, Chelsea, Manchester City na New York City.

No comments

Powered by Blogger.