Full-Width Version (true/false)


Gigy Money Aomba Radhi Baada Ya Kumchana X Wake Hadharani

Mwanamuziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameomba radhi baada ya ugomvi wake na Baba mtoto wake Mo J.

Gigy Money alimtolea maneno makali Ex wake ikiwemo kuweka wazi kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo kuwa mtoto wake Myra sio wa Mo J kwani alikuwa na mwanaume mwingine.

Gigy Money na Ex wake Mo J walirushiana maneno makali baada ya Gigy kumtuhumu kuwa hakuwa akimtunza kipindi cha ujauzito na kudai alihama na kila kitu baada ya kuachana.

Baada ya sakata hilo Mo J aliongea na vyombo vya habari na kudai kuwa ana uhakika kuwa mtoto wao ni wa kwake ingawa Gigy kwa ajili ya hasira anampa  mtoto mpenzi wake wa sasa.

Baada ya povu hilo Gigy Money ameibuka na kuomba radhi kwa maneno aliyoongea huku akidai ilikuwa ni hasira ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka ujumbe huu:


No comments

Powered by Blogger.