Full-Width Version (true/false)


Gombana na mke lakini sio mpenzi - Juma NatureMsanii mkongwe na miongoni mwa waasisi wa muziki wa BongoFleva, Juma Nature amefunguka na kudai haoni tija kwa wasanii wa sasa kutumia kiki za kugombana na wapenzi katika mitandao ya kijamii ili watengeneze njia ya kuachia kazi mpya. 

Nature ametoa kauli hiyo wakati wasanii wa muziki wa BongoFleva pamoja na ule wa kufokafoka 'hip hop' wa kizazi hichi kutumia kiki kama sehemu moja wapo ya kujitengenezea mazingira mazuri ya kuzungumziwa kwenye midomo ya watu ili mradi akitoa kazi yake mpya wadau wapate kusikiliza kwa wingi jambo ambalo linateketeza tasnia hiyo bila ya wao wenyewe kufikilia.

"Zile bifu za wasanii wa zamani zilikuwa zimekaa kisanii zaidi yaani zimetengenezwa licha ya kuwepo na lapsha mbili tatu, lakini sasa hivi bifu hamna, mimi nawaona watu wanagombana na wachumba, mademu zao tu vitu ambavyo naona kama vya kiduwanzi. Bora useme mtu na mkewe wanagombana labda tena hilo suala jingine kubwa", amesema Nature.

Pamoja  na hayo, Nature ameendelea kwa kusema "lakini ugomvi wa mtu na mchumba wake naona ni mambo ambayo hayana hata 'issue', ndio kiki zilizokuwepo kwa sasa lakini sioni kama zinawajenga".

Kwa upande mwingine, Nature amesema kama ni msanii anajiamini basi afanye kazi nzuri na awaache watu wasikilize ili wajue ni nani bingwa ambaye ataweza kuwakilisha hapa duniani.

No comments

Powered by Blogger.