Full-Width Version (true/false)


Haji Manara aipongeza Azam FC
Muda mfupi baada ya Azam FC kutangaza kumsajili mshambiliaji Donald Ngoma, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametupa 'dongo' la kuipongeza Azam FC kwa usajili huo pamoja na mchezaji mwenyewe husika. 

Manara ametumia ukurasa wake wa Instagram kueleza yale yaliyo moyoni mwake kwa kudai Ngoma hakuwa na tatizo la kiafya bali alikuwa na matatizo mengine nyuma ya pazia.

"Donald Ngoma na Azam fc wamemalizana rasmi...inavyoonekana Ngoma hakuwa mgonjwa wa afya bila shaka alikuwa mgonjwa wa kukosa mishahara, sijui hajalipwa miezi mingapi maskini ya 'God', kila la kheri kwako 'Striker' Donald Ngoma", amesema Manara.

Uongozi wa Azam FC ulitangaza kuingia makubaliano ya awali na mshambuliaji Donald Ngoma akiwa anatokea klabu ya Yanga SC ambapo alisajiliwa msimu wa ligi kuu 2017/2018 lakini hakufanikiwa kufanya vizuri kutokana na majeraha yaliyopelekea kuwa nje ya dimba kwa kipindi kirefu.

No comments

Powered by Blogger.