Harmonize amgeukia Diamond baada ya kuweka rekodi ya pekee Tanzania

Kauli ya muimbaji huyo inakuja mara baada ya wimbo huo kufikisha views milioni 10 katika mtandao wa YouTube kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kufanya hivyo.
“Pia naamini uwepo wa Diamond umechangia kwa sababu ninaamini kuna
sehemu muziki wangu haujafika, umefika kupitia Diamond pia,” amesema.
“So namshukuru ana mchango mkubwa licha ya verse ambayo amefanya
kwenye wimbo lakini pia image yake imetumika kusaidia,” Harmonize
ameiambia Wasafi TV.
Kwa Ngwaru ni wimbo wa pili kwa Harmonize kufanya na Diamond Platnumz
baada ya kutoa wimbo unaokwenda kwa jina la Bado uliotoka miaka miwili
iyopita.
No comments