Full-Width Version (true/false)


Harry Kane atangazwa nahodha timu ya Uingereza kombe la Dunia Urusi
Straika wa klabu ya Tottenham, Harry Kane ametangazwa kuwa nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kinachotarajiwa kushiriki michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi mwaka huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ameifungia klabu yake ya Spurs jumla ya mabao 41 kwenye michezo 48 msimu huu na magoli 12  kwenye mechi 23 za timu ya taifa.

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema kuwa maamuzi yake yamempedekeza Kane.

No comments

Powered by Blogger.