Full-Width Version (true/false)


Hitaji la Simba kombe lao wakabidhiweSingida lagonga mwamba

Wakati Simba ikiomba kupelekewa kombe la Ligi Kuu Bara mjini Singida, uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umesema haujapata barua ya Simba.

Kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, amesema kuwa hawajapata taarifa rasmi za Simba kuhitaji kupelekewa kombe hilo ili wakakabidhiwe baada ya mechi na Singida United kesho Jumamosi.

Wambura ameeleza kuwa kufuatia msimamo wa ligi ulivyobadilika jana, TFF itafanya mchakato wa kuikabidhi Simba kombe hilo baada ya mechi ya kesho.

Simba imetangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu baada ya Yanga kupoteza mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kwa mabao 2-0 na kuwafanya Simba waendelee kusalia kileleni wakiwa na pointi 65 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote.

Kauli hiyo kutoka bodi ya ligi imekuja kufuatia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, kuomba wapelekewe kikombe hicho ili wakakipokelee mjini Singida.

No comments

Powered by Blogger.