Full-Width Version (true/false)


Hizi ndio rekodi walizoweka Ronaldo na Messi
Wachezaji bora wa Dunia katika miaka 10 iliyopita Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, wameendelea kujiwekea rekodi zao mbalimbali baada ya wote kufunga kwenye mchezo wa El Clasco jana.

Baada ya kuifungia bao la pili timu yake jana, Messi alifikisha mabao 7 ya kuifungia Barcelona kwenye mechi za El Clasco katika La Liga hivyo kuivunja rekodi ya nyota wa zamani wa Barcelona Paco Gento aliyekuwa amefunga mabao 6.

Mbali na rekodi hiyo Messi pia amefikisha mabao 28 ya kuifunga Real Madrid na kuendelea kupanua wigo wa mabao katika mchezo wa El Clasco akimzidi Cristiano Ronaldo ambaye amefunga mabao 18 hadi sasa.

Wakati huo bao la kusawazisha la Cristiano Ronaldo lilimfanya nyota huyo kufikisha mabao 18 kwenye El Clasco na kuifikia rekodi ya nyota wa zamani wa Real Madrid Alfredo Di Stéfano ambaye alifunga idadi hiyo ya mabao.

Wakati huo Barcelona wameendelea kushikilia rekodi yao ya kutofungwa msimu huu ambapo sasa wamecheza mechi 35 za La Liga bila kupoteza na wamebakiza mechi 3 kumaliza msimu bila kufungwa eti hawataruhusu hilo.

No comments

Powered by Blogger.