Full-Width Version (true/false)


Hizi ndio takwimu muhimu kuelekea kufunga VPL leoIkiwa leo ndio siku ya kufunga msimu wa ligi kuu soka Tanzania Bara 2017/18, yapo mambo mbalimbali yakutazama. Pamoja na bingwa kupatikana ambaye ni Simba, lakini nafasi ya pili bado kitendawili kwa Yanga na Azam FC.

Timu zote 16 za ligi kuu leo zinaingia uwanjani kukamilisha mechi 30 kwa kila timu msimu huu ambapo pia zitakamilika mechi 240 za msimu huu ulioanza Septemba mwaka 2017.

Mechi 7 kati ya nane za leo zitacheza muda mmoja wa saa 10:00 jioni, huku mchezo mmoja kati ya Azam FC na Yanga ukichezwa saa 2:00 Usiku. Ni wazi mshindi wa mchezo huo atamaliza katika nafasi ya 2 msimu huu.

Kwenye mchezo huo Azam FC yenye alama 55, inahitaji sare tu ili kujihakikishia kumaliza katika nafasi ya pili. Yanga ambayo imepokonywa taji na Simba SC wana alama 52 na wanahitaji ushindi ili kufikisha alama 52 huku idadi ya mabao ikiwabeba kukaa katika nafasi ya pili.

Kwa upande wa timu za kushuka daraja tayari timu ya Njombe Mji imerejea ilikotoka baada ya kucheza ligi kwa msimu  mmoja. Timu ambazo zinaweza kuungana na Njombe Mji ni Ndanda FC ambayo leo inacheza na Stand United pamoja na Majimaji ambayo inacheza na Simba.

Msimu ujao ligi kuu itashirikisha timu 20 ambapo timu 6 zimepanda daraja msimu huu ambazo ni Biashara Mara, Alliance Schools na KMC. Nyingine ni Coastal Union, African Lyon na JKT Tanzania ambazo zimerejea baada ya kushuka misimu kadhaa iliyopita.
 

No comments

Powered by Blogger.