Full-Width Version (true/false)


Huruma,Yanga bado hali tete..yachapwa 1-0 na Mtibwa


 


Klabu ya soka ya Yanga imeendelea kupata matokeo mabaya tangu aliyekuwa kocha wao mkuu George Lwandamina, aondoke ambapo sasa imecheza mechi saba bila ushindi. 
Yanga leo imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa jioni hii kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro. Bao pekee la Mtibwa limefungwa na Hassan Dilunga dakika ya 82.

Mechi hiyo inakuwa ya tatu mfululizo kwenye ligi kwa Yanga kupata kipigo ambapo ilianza kwa kufungwa na Simba bao 1-0 na kisha kufungwa mabao 2-0 na Tanzania Prioson na leo imepata kipigo kutoka kwa Mtibwa.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga imeendelea kusalia kwenye nafasi ya 3 nyuma ya Azam FC na Simba ikiwa na alama 48 katika mechi zake 26 ilizocheza hadi sasa. Imebakiza mechi 4 kumaliza msimu huku Azam na Simba zikiwa zimebakiza mechi 2.

Kikosi cha Yanga kinarejea jijini Dar es salaam kesho, tayari kwa kuanza maandalizi ya mchezo wake wa pili kwenye hatua ya makundi dhidi ya Rayon Sports itakayopigwa Mei 16 kwenye uwanja wa taifa.

No comments

Powered by Blogger.