Full-Width Version (true/false)


Huyu ndio Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Quran


Mashindano  ya kumtafuta mwakilishi atakae wakilisha kimataifa katika mashindano ya Quran yamefanyika leo mei 18 katika Msikiti wa Kichangani uliopo magomeni Mikumi Jijini Dar es salaam.
Mashindano hayo yaliowashilikisha washiriki wanne ambapo ulifanyika mchujo kwa kusoma Quaran ili kumpata mshindi ambae ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kimataifa yatayofanyika tarehe 3 mwaka huu katika ukumbu wa diamond Jubilee.

Akitoa shukrani zake mara baada ya kuibuka kidedea kijana Aboubakar Muhammed Omar amesema kuwa Shindano lililkuwa gumu kutokana alikuwa na akichuana na watunwenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi Quran ambapo amewaomba watanzania kuendelea kumuombea Dua kutokana yeye ndiye anaekwenda kuiwakilisha Nchi.

Aidha amewashukuru Majaji ,marafiki  pamoja na walimu wake kwa kumuombea Dua huku akisistiza waendelee kuwa nae begaa kwa bega wakati wote wa mashindano.


"Suala la kuwakilisha nchi ni zuri lakini linahitaji sana msaada wa Dua ili kuweza kufikia malengo"Amesema Aboubakar

Kwa upande wake Mshiriki mwingine ajulikanae kwa jina la Ismail Ally Jumma kutoka Markaz ameeleza kuwa kilichompelekea kushindwa Shindano hilo ni kubadilika kwa sauti yake huku akidai ni Moja ya Changamoto za Swaum ambapo sauti yake ilibadilika ghafla kwa kukauka.

Mashindano hayo yameshirikisha wanafunzi wanne kutoka katika Madrasa tofauti nchini.

Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika Tarehe 03-06-2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee upanga jijini Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.