Full-Width Version (true/false)


Huyu Ndiye Muimbaji wa Injili Kenya Anayedaiwa Kupewa Ujauzito na HarmonizeMrembo kutoka nchini Kenya ambaye pia ni msanii wa muziki wa Injili, Veronica Wanja ‘Nicah The Queen’ anadaiwa kupewa ujauzito na msanii Harmonize.

Hata hivyo Nicah The Queen amekanusha taarifa hizo kwa kueleza kuwa hazina ukweli wowote, awali Nicah alikuwa katika mahusiano na mchekeshaji Dr. Ofweneke’s.


Taarifa za ndani zaidi kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa kipindi cha nyuma Nicah The Queen na Harmonize walikuwa wakionekana pamoja.
Weekend iliyomalizika Harmonize alikuwa nchini Kenya ambapo alitumbuiza katika show ya 10 Over 10 inayoruka kupitia Citizen TV.


Nicah The Queen hapo awali alitamba na nyimbo kama Pagawisha na Ushuhuda ila kwa sasa anafanya vizuri na wimbo unaokwenda kwa jina la Naringa. Unaweza kuutazama hapa chini.

No comments

Powered by Blogger.