Full-Width Version (true/false)


Ijue rekodi hii ya pekee kwenye VPLIkiwa ligi kuu ya soka Tanzania Bara inaelekea ukingoni ambapo baadhi ya timu zimebakiza mechi moja na zingine mbili, Klabu ya Ndanda FC ndio timu pekee ambayo imeshinda mchezo mmoja tu kwenye uwanja wake wa nyumbani. 
Ndanda FC ambayo imecheza mechi 28 hadi sasa, leo itashuka kwenye dimba lake la nyumbani (Nangwanda Sijaona) mjini Mtwara, kusaka ushindi wa pili kwenye wa nyumbani baada ya kufanya hivyo kwenye mechi dhidi ya Lipuli FC pekee.

Timu hiyo inayoshika nafasi ya 15 ambayo ni yapili kutoka mwisho ikiwa na alama 23, hadi sasa imecheza mechi 13 kwenye uwanja wa nyumbani na kufanikiwa kushinda 2-1 dhidi ya Lipuli FC pekee.

Mbali na kutoshinda nyumbani lakini timu hiyo imefanikiwa kushinda mechi za ugenini kadhaa zikiwemo 1-0 dhidi ya Mbeya City, 1-0 dhidi ya Stand United na 1-0 dhidi ya Majimaji FC.

Ndanda inahitaji ushindi pekee ili iweze kufufua matumaini ya kutoshuka daraja. Timu zingine ambazo zipo kwenye hatari hiyo ni Majimjai FC yenye alam 24 na Njombe Mji yenye alama 22.

No comments

Powered by Blogger.