Full-Width Version (true/false)


ILI KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA MWAKANI, YANGA INAPASWA KUBEBA UBINGWA CAF
Kikosi cha Yanga kinafanya mazoezi yake ya mwisho leo kuelekea mchezo wa pili wa hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports utakaopigwa kesho Jumatano.

Yanga itakuwa kibaruani kesho kupigania bahati nyingine kufuatia kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya USM Alger ya Algeria kwa mabao 4-0 ugenini.

Taarifa kutoka uongozi wa Yanga zinasema wachezaji wote wapo kwenye morali na hali nzuri kuelekea mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Yanga inahitaji kupata matokeo ili kujiwekea nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo kutokana nakufanya vibaya katika mtanange wa kwanza.

Tayari kikosi kilichokuwa Morogoro kwa mechi ya ligi, kimewasili Dar es Salaam kujiunga na wachezaji waliokuwa wamesalia jijini humo ili kuongeza nguvu ya maandalizi.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa moja za usiku jioni.

No comments

Powered by Blogger.