Full-Width Version (true/false)


Ilivyokuwa kesi ya Meneja TPA anaemiliki nyumba 23, magari 7


Leo May 3, 2018 Upelelezi wa kesi inayomkabili Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,(TPA), Prosper Kimaro ya kujilimbikizia mali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.4 zisizolingana na kipato chake bado haujakamilika.

Wakili wa serikali Mkuu, Vitalis Peter amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi June 5,2018, huku akiutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi.

Mshtakiwa huyo amefunguliwa kesi hiyo chini ya kifungu cha 27 (1)(4) cha sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kimaro anadaiwa kumiliki nyumba zenye thamani ya Sh.Bilioni 1.1 na magari  yenye thamani Sh. Milioni 307,364,678.20, zisizolingana na kipato chake ambapo anadaiwa ametenda kosa hilo kati ya mwaka 2012 na 2016.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa akiwa maeneo ya Temeke kama mtumishi wa umma wa TPA alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake halali cha zamani na  cha sasa.

Mali hizo ni nyumba mbili  zilizopo mtaa wa Uwazi Temeke zenye thamani ya Sh. 124.2 milioni,  kiwanja kilichopo Yombo Vituka chenye thamani ya Sh12.9 milioni.

Nyumba mbili zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh 63.5 milioni, nyumba tatu zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh 159 milioni.

Nyumba nyingine tatu zenye thamani ya Sh. Mil 170.1 nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.Mil 71.3 na kiwanja kilichopo Temeke chenye thamani ya Sh.Mil 35.

Pia kiwanja chenye thamani ya Sh.Mil 25 kilichojengwa nyumba tatu za Sh.Mil 159 pamoja na  nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.Mil 106.

Pia nyumba  zenye thamani ya Sh.Mil 214, Nyumba nne eneo la viziwaziwa Kibaha Mjini zenye thamani ya Sh 199.7 milioni na nyumba nyingine iliyopo Kilimahewa Tandika yenye thamani ya Sh 70 milioni.

Pia anamiliki magari aina ya Toyota Land cruise lenye thamani ya Sh 180.1 milioni, Mitsubishi lenye thamani ya Sh 38.4 milioni,  Massey Ferguson lenye thamani ya Sh  24 milioni na Trailer lenye thamani ya Sh 4.5 milioni.

Mengine ni  Toyota Harrier yenye thamani ya Sh 35.8milioni, Trailer lenye thamani ya Sh 4.8 milioni, na Massey Ferguson lenye lenye thamani ya Sh 19.1milioni.

No comments

Powered by Blogger.