Full-Width Version (true/false)


Jerry Muro na Haji Manara kupamba mechi ya Uwesu Cup


Baada ya mechi ya Simba SC na Yanga SC iliyochezwa weekend iliyopita na vijana wa Msimbazi kuondoka na ushindi wa goli moja, burudani imehamia wilayani Pangani ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, Juma Uweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, ameandaa kombe la Uwesu Cub ambalo litafunguliwa kwa mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga.

Mchezo huo inatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake kutokana na msemaji wa Simba, Haji Manara pamoja aliyekuwa msemaji wa Yanga Jerry Muro kuthibisha kuwepo siku hiyo.


Mgeni rasmi wa tukio hilo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.

Akiongea na waandishi wa habari mapema jana, Mwenyekiti wa Uzalendo kwanza, Steve amesema Jumamosi watakuwa wilayani humo kwaajili ya kuwaelimisha vijana juu ya kujitambua, kutumia fursa walizonazo mkoani humo, kama kutumia vipaji walivyonavyo ili kufanikisha malengo yao ya kimaisha.

Amesema kuwa vijana wengi huvunjika moyo kutokana na changamoto wanazozipitia bila ya kujua watazitatua vipi, hivyo kupitia kampeni yao ya Amka Kijana wataweza kuwapa elimu mbalimbali.

Mbali na elimu hiyo pia amesema siku hiyo kutakuwa na mtanange wa soka baina ya mashabiki wa timu ya Simba na Yanga na baadaye watatembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vilivyomo wilayani humo.

Amesema wasanii mbalimbali kama, Aunt Ezekiel, Flora Mvungi, Jaqueline Wolper, Duma, Johari, JB na wengine wengi. Tamasha hilo litakuwa la wazi na halitakuwa na kiingilio.

No comments

Powered by Blogger.