Full-Width Version (true/false)


Jeshi la polisi lampongeza Mange Kimambi "tunampongeza kwa kuwa amerudi kundini"
Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ametoa wito kwa vijana kuacha ushabiki bila kuchunguza madhara yake. 


Kamanda Mambosasa ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam ambapo amesema mnamo tarehe 26 Jeshi la Polisi liliwakamata vijana ambao walikuwa kwenye maandalizi ya maandamano ambayo yalihamsishwa kwa njia ya Mtandao na Mwanadada Mange kimambi lakini baadaya ya muda mfupi alianza kuipongeza serikali.

"Nawasihi vijana mnaotumia mitandao ya kijamii mnaposhabikia vitu angalieni madhara Yaan faida na hasara zake Kwani mnamo tarehe 26 tuliwakamata vijana waliokuwa wakijiandaa kwa maandamano ambapo mhamasishaji Mange kimambi badae akaanza kuipongeza Serikali. Mange ameendelea kuipongeza serikali nasi tunampongeza kwa kuwa amerudi kundini", amesema Mambosasa.

Mambo Sasa ameendelea kusema
"Mange alikuwa anapotosha ila watanzania walipompuuza sasa ametambua ni afadhali naye arudi kuipongeza serikali. Watu tuliowakamata kwaajili ya kufanya maandamano tuliwahoji na kisha kuwapa dhamana".

Sanjari na hayo Mambosasa amesema kuwa hali ya usalama Jijini Dar es Salaam imezidi kuimarika siku hadi siku.Kwa stori za town kama hizi owload app yetu iliyopo playstore,>>>BOFYA HAPA

No comments

Powered by Blogger.