Full-Width Version (true/false)


JESHI la Polisi Mbeya limepiga marufuku wafiwa kupanda kwenye malori


 

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limepiga marufuku mtindo wa malori ya mizigo kubeba watu wanaokwenda kwenye mazishi kwa maelezo kuwa kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Usalama BarabaraniMbali na kupiga marufuku malori kubeba wafiwa, aina hiyo ya usafirishaji imezuiwa pia na polisi hapa Mbeya kwa watu wanaokwenda ama kutoka minadani kwa maelezo kuwa kunaweza kusababisha ajali. 

Marufuku hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Musa Taibu, wakati wa mkutano wake na waendesha bajaji na bodaboda ambapo alitaka madereva hao wakawe mabalozi juu ya katazo hilo. 


Taibu alisema dereva atakayebainika kuendelea kusafirisha wafiwa kwa kutumia malori na magari madogo ya mizigo atakamatwa. Kamanda Taibu alisema ametoa katazo hilo kutokaka na uwepo wa ajali zilizotokana na watu kusafiri kwa mtindo huo na ongezeko la wakazi wa Mbeya kutumia usafiri huo. watumie usafiri unaokubalika kwa mujibu wa sheria". 

"Tunafahamu (wafiwa) wanakuwa kwenye matatizo lakini vyema kutumia usafiri elekezi ili kuondoa tatizo lingine.” Aidha, Kamanda Taibu alisisitiza kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto ya usafiri kwa maeneo ya vijijini, lakini hatakubali kuona au kusikia wafiwa wakitumia usafiri wa malori na badala yake uwepo utaratibu maalum wa kukodi magari ya abiria ili kuwasafirisha. 

Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Musa Taibu amewata madereva kuacha tabia ya uvutaji bangi wanapoendesha vyombo vya moto, ili kuepuka ajili za barabarani. 

Alisema serikali baada ya kutoa katazo la unywaji wa pombe aina ya viroba, wengi wao wameanza kuvuta bangi. Alisema kupigwa marufuku kwa viroba kumesaidia kupunguza ajali za barabarani, lakini sasa madereva wamekuja na kilevi kingine cha bangi. 

Wakizungumzia uvutaji bangi, waendesha bajaji na bodaboda Peter Mwakyusa na Justine Waya walidai madereva watumiao kilevi hicho wengi wao ni wale wafanyao kazi usiku. Mwakyusa alisema binafsi hajawahi kuvuta bangi wala kunywa pombe na kwamba tabia hiyo inafanywa na watu wasiotii sheria za usalama barabarani. 

“Mimi ni Dereva ambaye nafanya kazi yangu kwa kuzingatia kanuni ambazo nilifundishwa darasani," alisema Mwakyusa na kueleza zaidi: 

"Tangu nianze kazi hii sijawahi lipishwa faini au kukamatwa kwa makosa ya uvunjifu wa sheria, wapo baadhi yetu ambao tunawaita amsha popo ambao wanafanya kazi mpaka usiku wa manane (hao ndiyo wenye matatizo).”

No comments

Powered by Blogger.