Full-Width Version (true/false)


Jeshi latangaza siku 18 kwa wadaiwa

 

Mei 17, mwaka huu Rais John Magufuli, wakati akizindua Kituo cha Uwekezaji JWTZ kupitia Suma JKT kilichopo Mgulani, jijini Dar es Salaam, alitoa mwezi mmoja kwa taasisi na idara za serikali na taasisi binafsi zinazodaiwa na JWTZ kulipa madeni yao kabla ya msako wa kuwatafuta haujaanza. 

Katika tangazo lao la juzi kwenye gazeti moja la kila siku (sio Nipashe), Suma JKT iliwatangazia wote wanaodaiwa kulipa madeni yao yote kabla ya Juni 15. 

“Suma JKT linawatangazia wadaiwa wake wote waliokopa matrekta, zana za kilimo na waliopatiwa huduma ya ulinzi binafsi kupitia kampuni Suma JKT Guard, kulipa madeni yote kabla ya June Katika hafla ya uzinduzi wa kituo hicho siku hiyo, Rais Magufuli alisema baada ya mwezi mmoja vyombo vya ulinzi na usalama viwasake wote waliokiuka malipo. Awali, Mkuu wa Jeshi hilo, Jenerali Venance Mabeyo, alimweleza Rais Magufuli kuwa Jeshi linadai Sh. bilioni 38 ambazo zilitokana na uuzaji wa matrekta na Sh. bilioni 3.4 za ulinzi kupitia Shirika la Suma Guard. 

Jenerali Mabeyo alimweleza Rais kuwa walikuwa na mradi wa matrekta ambayo waliyagawa maeneo mbalimbali, lakini hadi sasa wanadai Sh. bilioni 38. 

Rais Magufuli alisema Jenerali Mabeyo ameeleza kuwa walikuwa na mradi wa matrekta ambayo waliyagawa maeneo mbalimbali, lakini hadi sasa wanadai Sh. bilioni 38. “Zilikuwa Sh. Bilioni 40, lakini sasa zimebaki Sh. bilioni 38 ambazo hazijaletwa, watu wamechukua matrekta wamefanya biashara lakini hawarudishi na baadhi waliyopewa zipo taasisi za serikali na watu binafsi lakini taarifa nilizonazo baadhi ya akaunti za matrekta haya nyingine zinaingia kwenye mifuko ya watu binafsi,” alisema na kuongeza: 

“Sasa ninawaomba na nitoe wito kwa wote waliochukua na wanaodaiwa madeni kwa kuchukua matrekta, nawapa mwezi mmoja, ndani ya mwezi mmoja wawe wamelipa na wasikiuke kutokana na makubaliano yaliyokuwapo kwenye mikataba yao,” alisema. 

Rais Magufuli alisema baada ya mwezi mmoja vyombo vya ulinzi na usalama viwasake wote waliokiuka. 

Rais Magufuli alisema badala ya watu kuzitumia fedha hizo anataka viwanda viende mbele ili jeshi lisihangaike kumuomba fedha. Aidha, Rais Magufuli aliagiza madeni ya Sh. Bilioni 3.4 ambayo Suma Guard inadai taasisi mbalimbali zikiwamo za serikali, wahusika wapelekewe taarifa. i 15,” alisema.

No comments

Powered by Blogger.