Full-Width Version (true/false)


Joe Hart atoa povu zito kwa kutemwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakachoshiriki kombe la dunia


Ndoto ya kila mchezaji wa soka katika kipindi hiki ni kuhakikisha anawekwa kwenye orodha ya kuitumikia timu yake ya taifa katika michuano ya kombe la dunia. Baada ya Jack Wilshere kutoa povu kwa kuachwa kwenye kikosi cha Uingereza, Joe Hart na yeye amefuata nyayo hizo.

Golikipa huyo ambaye alifanikiwa kucheza mechi nyingi kwenye hatua ya kufuzu kwenye kombe hilo adai kuwa ameshangazwa na tukio hilo la kutemwa kwenye kikosi hiko.

Hart amesema hayo kupitia ujumbe wake aliouandika kwenye mtandao wa Instagram. Kupitia mtandao huo kipa huyo ameandika:
Siwezi kusema uongo, ninashangaa. Baada ya miaka 2 ya kujaribu kutoka katika hali mbaya sana, hii ni vigumu kuchukua. Ninajivunia kuwepo katika graft na kucheza kila dakika katika mechi za kufuzu ni muhimu sana katika matokeo hayo. Najua kile ninacholeta kwa timu, lakini ni nini. Bahati nzuri kwa timu huko nje, wachezaji wanajua kwamba hata kama sitakuwa huko, nitakuwa na jezi yangu ya Uingereza kama shabiki kipindi hiki na kusupport yote. Hakuna hofu, nenda ukaipoteze. na kujigamba x

No comments

Powered by Blogger.