Full-Width Version (true/false)


JWTZ laanza kutoa mafunzo kwa kutumuia silaha kubwa.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia shule ya mafunzo ya kijeshi ya RTS kihangaiko  limeanza kutumia silaha kubwa za kijeshi ikiwemo vifaru mabomu na silaha zingine katika mafunzo ya askari wanafunzi lengo ikiwa ni kuwaongezea ujuzi askari katika matumizi ya silaha za kivita tangu wakiwa mafunzoni na kuwafanya kuwa makakavu. 

ITV ilika kwenye  paredi la kuhitimu mafunzo kwa askari wanafunzi kutoka shule ya kijeshi ya RTS Kihangaiko na kushuhudia matumizi ya silaha kwa askari wanafunzi. 

Akizungumza na askari  wanafunzi zaidi ya elfu mbili mwakilishi wa kamandi ya vikosi vya chini makao makuu ya Jeshi la wananchi Canali Claud Martine anasema  askari hao ni sehemu ya askari wenye bahati ya kupata mafunzo ya juu wakiwa bado wanafunzi hivyo wanapaswa kuthamini nafasi walizonazo. 

Mkuu wa shule ya Mizinga Canal Julias Gamboshi anasema mafunzo ya aina hii yana umuhimu mkubwa katika karne hii ya teknolojia za  juu katika majeshi. 

creditid: ITV

No comments

Powered by Blogger.