Full-Width Version (true/false)


KAGERA SUGAR YAIWEKEA MAZINGIRA MAGUMU NJOMBE MJI KUSALIA LIGI KUU KWA USHINDI WA 3-1
Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Kaitaba mjini Kagera kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao mnono wa mabao 3-1.

Mabao ya Kagera Sugar yametiwa kimiani na Japhary Kibaya (10'), Edward Christopher (56') na Japhet Makarai katika dakika ya 71.

Bao pekee la Njombe Mji limefungwa na Notikely Masasi katika dakika ya 21.

Matokeo hayo yanazidi kuiweka katika mazingira mabaya Njombe Mji ya kuelekea kushuka daraja msimu huu baada ya kuendelea kusalia mkiani ikiwa na pointi 26 pekee.

Ushindi kwa Kagera umekuwa na manufaa ya kuzidi kujihakikishia inasalia katika ligi msimu ujao kwa kujikusanyia alama tatu muhimu huku ikifikisha jumla ya pointi 31 ikiwa nafasi ya 10.

No comments

Powered by Blogger.