Full-Width Version (true/false)


Kaka yake Pogba abadilikiwa na wachezaji wenzake uwanjaniBeki wa club ya Genclerbirligi ya Uturuki Florentin Pogba ambaye pia ni kaka wa staa wa Man United Paul Pogba ameingia matatizoni baada ya kutoka uwanjani wakati game ikiendelea  huku timu yake ikiwa nyuma kwa goli 1-0.

Timu ya Genclerbirligi anayoichezea Florentin ilikuwa ikicheza dhidi ya Antalyaspor lakini hadi Florentin anatoka uwanjani Genclerbirligi  walikuwa nyuma kwa goli 1-0, hivyo baada ya kuanza kutoka uwanjani wachezaji wenzake wakakasirika.

Florentin Pogba alitoka uwanjani timu yake ikiwa imemaliza nafasi tatu za kufanya mabadiliko lakini alitoka akionekana anachechemea kitu amabacho wenzake hawakutaka kumuelewa kutokana na timu kulazimika kucheza pungufu ya mtu mmoja uwanjani.

Baada ya kitendo hicho cha kutokana nje wachezaji wenzake walimfuata kwa hasira na kuanza kumfokea, hata hivyo bado haijathibitika kama Florentin alitoka nje kwa kuwa majeruhi au la game ilimalizika wakipoteza mchezo huo kwa 1-0 na wao kwa sasa wapo nafasi ya 17 katika Ligi na wamesalia na michezo miwili tu wanatakiwa kupambana wasishuke daraja.

No comments

Powered by Blogger.