Full-Width Version (true/false)


Kama ulituma maombi ya "passport" uhamiaji Dar,taarifa hii ikufikie


Ofisi za Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, imewataka watu waliomba hati za kusafiria ‘Passport’ kwenda kuzichukua kwani kuna zaidi ya Passport 1288 za zamani.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa wa Uhamiaji mkoa wa DSM, Crispin Ngonyani amesema kuna ugoigoi wa watu kwenda kuchukua Passport zao.

“Kuna watu waliomba Passport ambapo zile za zamani bado zipo na zitatumika hadi January 2020, pia wapo waombaji wa Passport mpya za Kielektroniki lakini nao hawaji kuchukua,” amesema Ngonyani

Ngonyani amewataka Watanzania wafike katika Ofisi za Uhamiaji DSM kwa ajili ya kuchukua Passport zao bila matatizo na wasitume watu.

Pia kuhusu msongamano wa maombi ya Passport, Ngonyani amesema Ofisi ya DSM itafanyika uzinduzi wa kutoa Passport katika Ofisi za Uhamiaji DSM

No comments

Powered by Blogger.