Full-Width Version (true/false)


Kama wewe ni shabiki wa Mrisho Mpoto na Harmonize jiandae kwa tukio hili

Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akishirikiana na muimbaji kutoka WCB, Harmonize wametangaza kuwashirikisha mashabiki wa muziki wao katika kazi yao mpya inayokwenda kuandaliwa wiki hii.

Mpoto ambaye ametoa taarifa hiyo hakuweka wazi ni kazi ya aina gani lakini amewataka mashabiki wa muziki wake kujitokeza kwa wingi ofisini kwake siku ya alhamisi wiki hii kwaajili ya project hiyo.

“Huu ni mwaliko rasmi kwako kama mdau na mshabiki wa Mrisho Mpoto na @harmonize_tz @mwijaku tunakularibisha kwenye Vidio ya kihostoria itakayofanyika siku ya Alhamis,” aliandika Mpoto Instagram.

Aliongeza, “Fika kwenye ofisi za Mrisho Mpoto Kinondoni Mkwajuni asubuhi saa mbili utakuta Mabasi ya WCB Ingia kaa subiri Safari ya kwenda Airport ili twende Location wewe kama siyo Mtanzanzania kumbuka Passport yako…ukiwa umevaa kiafrica…pendeza sanaaaaaa piga nummber ‭0717 027 457‬ kuthibitisha ujio wa Safari yako,”

Wadau wa mambo wamedai huwenda hiyo ikiwa ni project ya wimbo mpya ambayo inawashirikisha wasanii hao wawili maarufu nchini Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.