Full-Width Version (true/false)


Kanye West Anena kwa mara ya kwanza kuvamiwa kwa Kim Kardashian, Paris

Kim Kardashian hatowezakusahau tukio la kuvamiwa mjini Paris kaika tukio la mwezi Oktoba 2016. Kanye West amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo.

Akiongea na mtangazaji Charlamagne, Rapper huyo amesema kuwa alimfuata Kim mjini humo kwa ajili ya kumlinda na kuongeza kua watu walikuwa wamewepanga mikakati ya kufanya tukio hilo kwa muda mrefu. 

“Hali ya mke wangu Paris na mambo yote ya hisia ya kuwa na wasiwasi, hisia kama vile unaweza kufanya nini? Nilikwenda Paris kwa safari hiyo ili kumlinda, si kumlinda kimwili, lakini nilikwenda kumsaidia tu kwa kumuangalia,” amesema Kanye. 

“One of the things she said she heard was that they were coming to rob her and they had to wait until I had left. The people had been strategizing and scheming on that for a long time,” ameongeza. 

Inadaiwa kuwa tukio hilo la kuvamiwa kwa Kim na majambazi hao lilichukua takriban dakika 6 tu. Majambazi hao walichukua mikufu, pete, simu, credit cards na vitu vingine vinavyofikia thamani ya dola milioni 10.

No comments

Powered by Blogger.