Full-Width Version (true/false)


Kazi hii ni ngumu inahitaji maombi – Rais MagufuliRais Dkt John Magufuli amewataka wananchi kuendelea kumuombea kwani kazi ya urais ni ngumu inahitaji maombi na kuwataka waumini wa dini kiislamu kumuweka katika maombi hasa katika kipindi cha kuelekea katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 
Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 15, 2018 alipokuwa anaongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kukagua shehena ya mafuta ya kula ambayo yalikua yamezuiliwa bandarini hapo.

“Mama lishe na vijana mnaofanyakazi nipo pamoja na ninyi, mimi ni yuleyule Magufuli sijabadirika, muendelee kuniombea kazi hii ni ngumu sana ndugu zangu, inahitaji maombi hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ndugu zangu waislamu mniweka kwa Mola muendelee kuniombea, Mungu awabariki sana nawashukuru sana”, amesema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Magufuli ameagiza Waziri wa Fedha na Mipango na Waziri wa Viwanda kupeleka muswada Bungeni kurekebisha sheria ya tozo ya mafuta yanayoingia nchini.

“Tulifanya makosa mengine upande wa serikali bei ya mafuta ya kula na yale ya crude yote yanatozwa bei moja, nimewaeleza Waziri wa Fedha na Wizara ya Viwanda wakafanye marekebisho Bungeni, tunataka tujue kama ni crude, refined au double refined, tunataka tuimarishe viwanda vyetu ili watanzania wengi wapate ajira” aliongeza Dkt Magufuli.

Katika ziara ya kusthukiza ya Rais Magufuli bandarini hapo amebaini baadhi ya udanganyifu unaofanywa bandarini hapo ikiwemo kukuta matenki manne yaliyokuwa na malighafi ya kutengenezea sabuni tofauti na taarifa za awali ambazo zilisema kuna mafuta ya kula.

Kwa siku za karibuni kumekuwepo hali ya sitofahamu baada ya meli mbili zenye shehena ya mafuta yaliyoagizwa na wafanyabishara yenye jumla ya uzito tani 40,000 iliyozulilwa bandarini baada ya ukinzani wa taarifa kati ya Shirika la viwango nchini (TBS) waliodai mafuta hayo ni ghafi wakati upande wa mamlaka ya mapato (TRA) ikidai mafuta hayo ni safi na yanastahili kutozwa kodi 25%

No comments

Powered by Blogger.