Full-Width Version (true/false)


Kesi ya Malinzi ngoma bado kabisa


Dar Kesi ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji inayomkabili, aliyekuwa Rais TFF, Jamal Malinzi (57), na wenzake wanne imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu.es Salaam. Kesi ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji inayomkabili, aliyekuwa Rais TFF, Jamal Malinzi (57), na wenzake wanne imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu.

Kesi hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017, iliyopo katika hatua ya usikilizwaji, imeshindwa kuendelea  baada ya Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Wilbard Mashauri kuwa Mahakama Kuu.

Wakili wa Takukuru, Leonard Swai alidai Mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Matha Mpanze, wakati shauri hilo lolipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

"Washtakiwa wote wapo mbele ya mahakama yako na kesi hii ilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka, lakini hakimu anayesikiliza  shauri hili yupo Mahakama Kuu, hivyo tuaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea" alidai Swai.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mpanze aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 11,mwaka huu itakapoendelea na usikilizwaji.

Mbali na malinzi, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine(46), Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga(27), Meneja Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya.

Katika mashtaka hayo, Malinzi anakabiliwa na mashtaka 28 ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 naSh 43,100,000.

Mwesigwa anakabiliwa na mashtaka sita  ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi,  na utakatishaji wa fedha.

Kwa upande wa mshtakiwa Nsiande anakabiliwa na mashtaka mawili ya utakatishaji wa fedha, mshtakiwa  Zayumba yeye  anakabiliwa na mashtaka  tisa ya kughushi na Frola anakabiliwa na shtaka moja la kughushi.

Hata hivyo, washtakiwa walikana mashtaka yanayowakabili, Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kuwa wanakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha huku wenzao Zayumba na Frola wapo nje kwa dhamana.

Tayari mashahidi wawili wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi wao akiwemo, Ofisa Mtendaji Mkuu Wa bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira Wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura (49)

Katika ushahidi wake, Mei 21, 2018, Wambura alidai kuwa  Muhtasari wa  Juni 5,2016 uliokuwa na ajenda ya kubadilisha watia saini Wa akaunti za benki za TFF zilizopo Stanbic benki  ni Wa kughushi na kwamba yeye haufahamu.

Alieleza kuwa anasema hayo kwa sababu alikuwepo katika kikao hicho cha Juni 5, 2016 na hakukuwepo na ajenda ya kubadilisha watia saini wa  benki Wa TFF kwa kumtoa Edgar Masoud na kumuingiza Nsiande Mwanga.

Alidai kuwa Edgar Masoud alikuwa ni Mkurugenzi Wa Fedha naUtawala TFF lakini kwa sasa ni marehemu na kwamba alifariki mwaka 2017.

Akitoa  ushahidi Wambura alidai kuwa  mchakato huo ulitakiwa kupelekwa kama ajenda ukieleza sababu za kutaka kufanya mabadiliko ya watia saini katika kamati tendaji ambapo ikiridhia mabadiliko hayo yanafanyika.
Alibainisha kuwa baada ya kupitishwa kwa mapendekezo hayo ina maana muhtasari huo unaenda kuitishwa katika kikao kinachofuatia kwa ajiri ya kuthibitishwa kuwa ndiyo uamuzi uliofanyika.

Alidai  kuwa yeye alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu Wa bodi ya ligi tangu Juni 2015 na majukumu yake yalikuwa ni kusimamia shughuli za ligi pia ni mjumbe sekretarieti ya TFF vinafanyika sekretarieti chini ya katibu Mkuu inachukua muhtasari ambao unawasilishwa katika kikao kinachofuata kwa ajili ya kuthibitishwa na kusainiwa na Mwenyekiti ambaye ni rais  Wa TFF, ama Makamu Wa Rais.

Alidai 2016 aliyekuwa mwenyekiti ni Jamali Malinzi  hats hivyo Wakili Kimaro alimuonyesha shahidi huyo  muhtasari Wa Juni 5,2016 ukimuonyesha yeye ni miongoni mwa wajumbe wa sekretarieti waliohudhuria katika kikao hicho.

Baada ya kuoneshwa na kuupitia muhtasari huo, Wambura alidai kuwa muhtasari huo wa Juni 5,2016 umeghushiwa na kwamba yeye haufahamu  kwa sababu alikuwepo katika hicho kikao na kwamba hakukuwapo na ajenda kubadilisha watia saini Wa TFF.ambayo inawezesha vikao vya kamati tendaji  kufanyika.

Wambura alidai kuwa kwa mujibu Wa katiba ya TFF  vikao  vinne  vinatakiwa kufanyika kwa mwaka na pale inapotokea dharura, panapotokea mahitaji.

"Mwaka 2016 kamati tendaji  ilikuwa na wajumbe wasiopungua 20 na wasiozidi 24 na kwamba utaratibu wa ufanyaji vikao kinaitwa na Mwenyekiti na kuwapelekea ajenda wajumbe." Alieleza Wambura.

Alidai kuwa nyaraka za ajenda zinaandaliwa na sekretarieti chini ya Katibu Mkuu na rais ambaye ndiyo msimamizi Wa sekretarieti.
Wakati vikao
     
     

No comments

Powered by Blogger.