Full-Width Version (true/false)


Kessy: Yanga tutarudi upya msimu ujao

 


Beki wa Yanga, Hassan Kessy ameweka wazi mapito yao msimu huu yatawafanya wawe bora mwakani, akiamini yataongeza juhudi ya umakini kwa kila idara. 

Kessy anasema mhitaji anapokosa kitu anatafuta kwa bidii ili aweze kukipata, tofauti na anayemiliki akidai anaamini mwakani watakuja kivingine. 

"Kama wachezaji tuliweza kupambana kadri tulivyoweza, lakini soka ndivyo lilivyo ingawa tulitamani hata tuishie nafasi ya pili imeshindikana. 

"Binafsi machungu huwa yananifanya nijitume zaidi ili kesho nimiliki, naamini msimu ujao hata viongozi wa Yanga watafanya jambo la kufanya ushindani uwe mkali," anasema Kessy.

No comments

Powered by Blogger.