Full-Width Version (true/false)


Kichuya aitumia salamu Singida United ‘tunazihitaji hizo pointi tatu’


Winga wa klabu ya Wekundu wa Msimbazi, Shiza Ramadhani Kichuya amewaambia wapinzani wao timu ya Singida United kuwa wanachokihitaji kutoka kwao ni pointi tatu muhimu na wala wasitarajie watakwenda ‘kurilaksi’ kwenye mchezo wao wa siku ya Jumapili kwakuwa wamesaliwa na alama moja pekee ili kutawazwa kuwa mabingwa wapya.

Kichuya ameyasema hayo kipindi hiki ambacho wamesaliwa na alama moja tu ili timu yake ya Simba kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu.
Haina haja ya ‘kurilaksi’ sisi tunahitaji kutafuta pointi tisa ya hizo mechi tatu ambazo zimebaki. Kwahiyo hatwendi ‘kurilaksi’ tuna kwenda kutafuta alama tatu alafu tubakize hizo mechi mbili kwasababu sisi matarajio yetu ni kumaliza ligi tukiwa hatujafungwa hata mchezo mmoja ahadi ndiyo hiyo wasifikirie sisi bado alama moja wakajua tutakwenda ‘kurilaksi’.
Simba yenye jumla ya pointi 65 wanatarajia kushuka dimba la Namfua kuwakabili Singida United mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara utakao pigwa siku ya Jumapili ya Mei 12 huku vijana hao wa msimbazi wakihitaji alama moja tu kuwa mabingwa wapya msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.