Full-Width Version (true/false)


Kigwangalla atoa magari kwa Wabunge 6Katika kukabiliana na tatizo la Ujangili nchini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amekabidhi magari 6 kwa Halmashauri sita tofauti yatakayotumika kwa ajili ya kupambana na vita hiyo. 
Kwa niaba ya Halmashauri hizo, Kigwangalla amewakabidhi magari hayo Wabunge kwenye ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini  Dodoma.

Wabunge waliokabidhiwa magari hayo ni wa  Bunda Vijijini Boniface Getere, Mbunge wa Itilima Njalu Silanga, mbunge wa Longido Dk. Steven Kiruswa, Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay na Mbunge wa Tanganyika Moshi Kakoso.


Kwa upande wake Mbunge wa Ngorongoro, William Ole Nasha hakuweza kufika kutokana na kubanwa na majukumu mengine katika Wizara yake ya Elimu lakini atakabidhiwa atakapofika ofisini hapo.

Waziri Kigwangalla amesema wamekabidhi magari hayo kwa wilaya hizo kwa kuzingatia sifa na mahitaji kwasababu zipo pembezoni mwa hifadhi mbalimali za taifa hivyo uwepo wa magari hayo utarahisisha zoezi hilo.

No comments

Powered by Blogger.