Full-Width Version (true/false)


Kikosi cha Mabingwa wa soka nchini Yanga, kimeondoka jijini Dar es Salaam mchana huu kuelekea jijini Mbeya, tayari kwa mchezo wa Ligi kuu kesho dhidi ya Tanzania Prison huku ikiwa kwenye mtego wa ubingwa wa Simba. 


Yanga imewasili jana ikitokea nchini Algeria ilikocheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger lakini imeunganisha leo kuwahi mchezo wake huo wa kesho ambao msemaji wa Yanga Dismas Ten amesema wanauchukulia kwa umuhimu wake.

Yanga inakwenda Mbeya ikiwa kwenye mtego wa kutoa ubingwa kwa Simba endapo itatoa sare au kufungwa kwenye mchezo huo itakuwa imevua rasmi taji la ligi kuu baada ya kudumu nalo kwa misimu mitatu mfululizo.

Simba kwasasa inahitaji alama moja tu kuweza kuwa bingwa msimu huu hivyo inaweza isisubiri mchezo wake wa jumamosi na Singida United ili ianze kusherehekea ubingwa bali inaweza kufanya hivyo kesho ednapo Yanga itakosa ushindi.

Mchezo huo wa kesho utapigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini humo. Yanga kwasasa ina alama 48 kwenye mechi 24 huku Simba ikiwa na alama 66 kwenye mechi 27.

No comments

Powered by Blogger.