Full-Width Version (true/false)


Kikosi cha Uingereza chaanza mazoezi rasmi kuelekea michuano ya kombe la Dunia

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amekiongoza kikosi chake kwenye mazoezi ya kwanza mapema hii leo kuelekea michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi.Jumla ya vijana 23 wanaounda kikosi cha Uingereza wamewasili kwenye viwanja vya St George’s Park hapo jana siku ya Jumatatu sehemu ambayo ndiyo kituo cha mazoezi ya timu hiyo ya taifa.Dele Alli na nahodha wa timu hiyo, Harry Kane ni miongoni mwawachezaji waliyofanya mazoezi ya kwanza hii leo siku ya Jumanne.Kinda wa Chelsea, Mason Mount, kiungo wa Watford, Nathaniel Chalobah na mlindalango wa Manchester City, Angus Gunn wameshiriki mazoezi hayo.

Wachezaji nane wa Uingereza wanahusishwa kujiunga na kikosi kwenye mazoezi St George Park wakati mchezaji wa Manchester City, Raheem Sterling akikosekana kufuatia kuwa na matatizo binafsi.Beki wa Chelsea, Gary Cahill na mchezaji wa Manchester United, Phil Jones, Ashley Young, Jesse Lingard pamoja na Marcus Rashford wakitarajiwa kuwasili Alhamisi baada ya kupewa mapumziko ya muda kufuatia kutoka kwenye mchezo wa fainali wa michuano ya kombe la FA Cup.

Wakati huo wachezaji wa Liverpool, Jordan Henderson na Trent Alexander-Arnold wakitarajiwa kujiunga na timu mwezi ujao kwakuwa kipindi hiki wanajiandaa na mchezo wa fainali kombe la klabu bingwa barani Ulaya Mei 26 dhidi ya Real Madrid.

No comments

Powered by Blogger.