Full-Width Version (true/false)


“kila lenye mwanzo lina mwisho”-KinanaAliyekuwa katibu mkuu Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema katika majukumu ya mwanadamu ni lazima kuwe na muda wa kufanyakazi na kupumzika na hakuna jambo lisilo kuwa na mwisho. 

Kinana amesema hayo leo Mei 28, 2018 katika kikao cha wa halmashauri kuu Taifa CCM (NEC) katika ukumbi wa mikutano Ikulu Jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza kustaafu nafasi ya Ukatibu Mkuu wa chama hicho na kuongeza kuwa anashukuru wanachama na viongozi wa chama hicho kwa ushirikiano kwa kipindi cha uongozi wake.

“Lazima tukubali kuna wakati wa kufanyakazi na wakupumzika, naelewa ugumu mnaoupata wa kutokunikubalia, tumekuwa na makatibu wakuu saba kwahiyo sio ajabu katibu mkuu wa sasa kuanchia ngazi ili apatikane mwingine, nashukuru mwenyekiti, makamu mwenyekiti na mzee Mangula kwa kunikubalia na kutambua kuwa kila lenye mwanzo lazima liwe na mwisho”, amesema Kinana.

Kinana ameongeza kuwa amepokea simu na ujumbe mwingi katika simu yake za wanachama na viongozi wa chama hicho wakimtaka kuendelea na nafasi ya ukatibu mkuu.

Katika upande mwingine kikao hicho cha Halmashauri kuu Taifa (NEC) kimefanikiwa kuchagua wajumbe sita kutoka Zanzibar na Tanzania bara kuingia katika kamati kuu ya Halmashauri kuu ambapo Afadhali T. Afadhali, Kombo H. Juma na Lailah B. Ngozi ni wajumbe kutoka Zanzibar na wajumbe kutoka Tanzania bara ni Mizengo Pinda, Charles Makongoro Nyerere na Khadija Taya maarufu kama Keisha.

No comments

Powered by Blogger.