Full-Width Version (true/false)


Kilichosababisha kesi ya Tido Mhando kushindwa kuendelea leo

 

Leo May 18, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando baada ya shahidi kupata udhuru.

Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa  mashahidi wa upande wa mashtaka.

Hata hivyo, wakili Swai amedai kuwa shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi ktika kesi hiyo anaudhuru.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi June 8, 2018 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wamekwishatoa ushahidi  wao ambao ni Afisa uchunguzi wa TAKUKURU, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Shilingi Milioni 887.1.

No comments

Powered by Blogger.