Full-Width Version (true/false)


Kinachoendelea Shule ya Msingi Mitambo

 Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Mtwara Bwana Sudi Abduli amesema kwamba ujenzi wa vyumba vya madarasa 8 katika shule ya msingi mitambo unakaribia kukamilika, na wanafunzi wataondokana na tatizo la kusomea nje.
tayari vyumba viwili kati ya 5 ambavyo vilikuwa vinakosekana vimeshakamilika, na vitatu vilivyosalia vimefikia kwenye rinta, na baada ya muda mfupi shule hiyo itakuwa imeondokana na tatizo lamukosefu wa madarasa kama ambavyo hapo awai ilikuwa.

Ujenzi unaendelea, kulikuwa na madarasa matatu kulikuwa kunakosekana vyumba vitano, kati ya hivyo vitano viwili vimeshakamilika, na vitatu vinaendelea vimefikia ngazi ya rinta, mpaka baada ya mwezi mmoja ujao au miezi miwili ijayo madarasa yote 8 yatakuwa yamekamilika”, amesema Sudi Abduli

Kwa mujibu wa Kaimu Afisa Elimu huyo amesema ujenzi huo umefanikishwa na wananchi wenyewe kujitolea, halmashuri ya wilaya, program ya EP4R na hamasa iliyotolewa na mkuu wa mkoa Mtwara.
Baadhi ya majengo ya shule ya msingi Mitambo

No comments

Powered by Blogger.