Full-Width Version (true/false)


Kiongozi Yanga amtetea Kelvin Yondan,Aituhumu Azam TV kwa upendeleo


Salum Mkemi


Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga, Salum Mkemi amewacharukia Azam TV akiwalaumu kutokutangaza kitendo cha Kelvin Yondani kutemewa mate wakati wa mchezo wa Yanga SC dhidi ya Singida United uliofanyika Uwanja wa Namfua.
Mkemi amehoji iweje Azam TV hawajatilia nguvu kutangaza tukio hilo huku akieleza kuwa wao na Simba baba  yao ni mmoja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mkemi amewauliza Azam TV kuwa Camera zao zilikuwa wapi wakati tukio hilo linafanyika? Ina maana hawakuliona hilo?

"Kunya anye kuku tu @hajismanara  @tanfootball @azamtvtz Hii haikushabikiwa wala hamkuitangza kwakuwa nyinyi na Simba baba yenu mmoja @azamtvtz hii kamera zenu haikuona siyo?." aliandika Mkemi.Kauli hiyo ya Mkemi imekuja kuafuatia tukio la beki Yondani lililo gumzo hivi sasa mitandaoni kumtemea mate mchezaji, Asante Kwasi, katika mchezo dhidi ya watani zao wa jadi Simba uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi Jumapili.

No comments

Powered by Blogger.