Full-Width Version (true/false)


KIONGOZI YANGA AOMBA WANACHAMA WAENDE NA ELFU THELATHINI KWENYE MKUTANO ILI ZIKAFANYE USAJILI
Katibu wa mipango wa zamani wa klabu ya Yanga, Abdul Sauko, amewaomba wanachama wa klabu hiyo kujitahidi walau kwenda na kiasi cha shilingi 30,000 katika mkutano mkuu utakaofanyika Juni 10 2018.


Sauko ambaye aliwahi kuwa kiongozi ndani ya Yanga ametoa ushauri huo kwa wanachama kwenda na kiasi hicho cha fedha ili zikaweze kutumika kwa ajili ya kufanyia usajili wa wachezaji.


Akizungumza kupitia Radio EFM katika kipindi cha Sports HQ, Sauko ameeleza kuwa klabu yao inapitia wakati mgumu kiuchumi hivi sasa huku akisema hakuna mwingine atakayeweza kuikoa zaidi ya wanachama wenyewe.


Mbali na kusaidia suala la usajili, Sauko pia amependekeza wanachama wabebe fedha hiyo itakayoweza kutumika kwa mambo mengine ya klabu kutokana na tatizo la kuyumba kiuchumi linaloikabili Yanga kwa sasa.


Yanga inaenda kufanya mkutano huo ambao awali ulipangwa kufanyika tarehe 16 Juni 2018, siku ambayo inaweza ikawa ni sikukuu ya Idd hivyo ikabidi urudishwe nyumba mpaka tarehe 10 Juni.

No comments

Powered by Blogger.