Full-Width Version (true/false)


Kitaifa » UONGOZI YANGA WAZIDI KUPIGA DANADANA KUHUSIANA NA KUONGEZA WACHEZAJI KWA AJILI YA KOMBE LA SHIRIKISHO


Uongozi wa klabu ya Yanga umezidi kupiga danadana kuhusiana na kuongeza wachezaji watatu watakaokipa nguvu kikosi chao kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kupitia Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa, amesema kuwa bado hawajafikia maamuzi ya kuweka wazi wachezaji ambao wamepanga kuwaongeza kikosini na muda utakapofika watawataja rasmi.

Kwa mujibu wa radio One kupitia Spoti Leo, Mkwasa ameeleza kuwa kwa sasa wanamalizia mechi za ligi ikiwamo ya leo dhidi ya Ruvu Shooting na itakayofuata watacheza na Azam FC.

"Bado hatujatoa taarifa rasmi kuhusiana na wachezaji hao, wakati mwafaka ukifika tutafanya hivyo, nawomba muendelee kusubiri" alieleza Mkwasa.

No comments

Powered by Blogger.