Full-Width Version (true/false)


Klopp awapiga kijembe Real Madrid ‘Uzoefu sio kilakitu’Meneja, Jurgen Klopp amesema kuwa wapinzani wake klabu ya Real Madrid wanawazidi Liverpool kwa uzoefu kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya lakini haimaanishi kuwa ndiyo kila kitu.

Wakati Liverpool ikitarajia kuwakabili Mabingwa wa Ulaya mara mbili mfululizo Real mchezo wa fainali siku ya Jumamosi huko Kiev, Klopp amesema kuwa na uzoefu hakumaanishi ndiyo kilakitu kwenye mchezo wa soka hicho kitu hakina umuhimu sana ila kuwa na matamanio na juhudi kwa kile unacho kihitaji ndiyo jambo la muhimu zaidi.
Wenzetu wanauzoefu zaidi na kama kungekuwa na duka la kuuza huo uzoefu basi Madrid sasa wangekuwa matajiri.

Uzoefu ni kitu muhimu kwenye maisha lakini sio kitupekee kwenye maisha hususani kwenye soka. Kunafaida ya kuwa na uzoefu lakini unaweza kukosa matamanio, tabia na hamasa ya kazi.
Wakati Madrid wakihitaji kutwaa taji hili kwa mara ya tatu mfululizo, Klopp anaamini atawazidi uwezo wapinzani wake ambao wanajivunia uzoefu waliokuwa nao pindi watakapo kutana Olympic Stadium.

No comments

Powered by Blogger.